Katika tunzo za BET AWARDS June 26, Future, Usher, na
Bryson Tiller wametangazwa kuongezwa kwenye orodha ya wasanii watakaotumbuiza
siku hiyo. Wanaungana na mastaa wengine waliokuwa wametangazwa awali ambao ni
pamoja na Alicia Keys, Maxwell, pamoja na tribute ya Prince itakayotolewa na
D’Angelo, The Roots na Janelle Monáe.
Mastaa watakaokabidhi tuzo ni pamoja
na DJ Khaled, Gabrielle Union, Tinashe, Fantasia, Regina Hall, Birdman,
Jermaine Dupri, Dame Dash na Snoop Dogg.
Diamond ni miongoni mwa wasanii
wanaowania tuzo hizo mwaka huu kwenye kipengele cha Best International Act:
Africa.
Washereheshaji wa show hiyo watakuwa
ni Anthony Anderson na Tracee Ellis Ross.
Tuzo hizo zitatolewa June 26 live
kutoka Microsoft Theater, Los Angeles, Marekani.



No comments:
Post a Comment