Azam yajitabiria mchuano mkali dhidi ya Simba Kesho - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, January 27, 2017

Azam yajitabiria mchuano mkali dhidi ya Simba Kesho

Wababe wa Kombe la Mapinduzi Azam FC wametabiri mchezo wao dhidi ya Simba kesho hautakuwa rahisi kwa kuwa timu zote ziko vizuri na zinataka pointi tatu.

Akizungumza  jana Kocha Msaidizi wa Azam, Idd Cheche alisema Simba ni timu nzuri na ina kikosi kizuri kama ilivyo kwa wao hivyo mchezo utakuwa mgumu.

Alisema muhimu kwao wa najipanga kushinda na kuchukua pointi hizo kama ilivyokuwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ambapo walishinda bao 1-0 katika mechi ya fainali.

“Maandalizi yetu yanakwenda vizuri na mpaka sasa hakuna majeruhi. Tunawajua Simba ni wazuri na hata sisi tuko vizuri, tunasubiri siku hiyo tuchukue pointi tatu,” alisema.

Cheche alisema hawana presha yoyote kuelekea kwenye mchezo huo kwani wanajua mbinu za wapinzani wao.

Mechi hiyo ni ya kisasi kwa kila mmoja baada ya kukutana katika mechi mbili huku kila upande ukimtambia mwenzie mara moja.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza Ligi Kuu Tanzania bara, Simba ilishinda bao 1-0 kwenye uwanja wa Uhuru.

Pia, Azam ikashinda 1-0 dhidi ya Simba kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi matokeo hayo yanaonesha ugumu wa mechi hiyo.

Hata hivyo, Simba ndiyo yenye presha kubwa katika mechi hiyo ya kesho kwani itahitaji ushindi ili iendelee kuongoza msimamo wa ligi, sare ama kupoteza kutaifanya izidi kupotea na kutoa nafasi kwa mpinzani wake Yanga itakayocheza na Mwadui keshokutwa. Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 45 na Yanga ni ya pili ikiwa na pointi 43 huku Azam ikishika nafasi ya tano ikiwa na pointi 31.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot