Dr. Harrison Mwakyembe, waziri wa katiba na sheria |
Na Francis Michael.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk
Harrison Mwakyembe amesema jumla ya watuhumiwa 30 wa mauaji ya vikongwe na
wenye ulemavu wa ngozi (albino) nchini, wamehukumiwa kunyongwa, baada ya
kupatikana na hatia ya mauaji hayo.
Dk
Mwakyembe amesema pia kuwa serikali itaendelea kutoa adhabu kali kwa watu
watakaobainika kuendelea kuhusika na mauaji ya watu hao ili kumaliza tatizo
hilo, ambalo limeipaka matope Tanzania kwa kuonekana sio kisiwa tena cha amani.
Waziri huyo alisema hayo mjini Shinyanga jana, alipofanya ziara yake ya kikazi.
Alisema
katika miaka ya hivi karibuni tatizo la mauaji ya wenye ualbino na vikongwe
yamepungua nchini na kwamba watahakikisha wanayakomesha kwa kutoa adhabu kali
kwa wauaji.
“Tatizo
hili la mauaji ya vikongwe na albino linatutia sana doa nchi yetu kimataifa
ambayo imekuwa ikisifika kwa amani na utulivu, hivyo natoa mwito kwa wananchi
waachane na mauaji ya watu hawa wasio na hatia pamoja na mahakama zifanye kazi
kwa kutoa hukumu za haraka kwa watu watakaohusika na mauaji hayo,” alisema Dk
Mwakyembe.
Hata
hivyo, Dk Mwakyembe alisema serikali itaanza mikakati ya kujenga mahakama za
mwanzo kwa kila kata nchi nzima ili kuondoa misongamano za kesi mahakamani na
kukarabati majengo ya mahakama ambayo yamechakaa.
Aliwataka
wakuu wa wilaya, waunde kamati za maadili ya wilaya.
Akisoma
taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack, alitaja changamoto
ambazo zinawakabili kuwa ni uchakavu wa majengo ya mahakama, uhaba wa mahakimu
na magereza ya Shinyanga na Kahama kuwa finyu na hivyo kusababisha mlundikano
wa wafungwa.
No comments:
Post a Comment