Mayai ya mwanamke |
Mwanamke ambaye anataka kutumia
mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi
mahakanani na kuruhusiwa kufanya hivyo.
Bintiye ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa kumuambia mamake amzalie watoto wake. Lakini mamake alishindwa katika kesi mwaka uliopita.
Mayai ya mwanamke yakifanyiwa urutubishaji |
Hata hivyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa mjini London mbele ya jopo la majaji watatu.
Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa mayai hayo hayangetolewa mjini London, kwa sababu bintiye hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili wa mama huyo waliwaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya bintiye ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment