Trump, Kagame Uso kwa uso - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, January 27, 2018

Trump, Kagame Uso kwa uso


Rais wa Marekani, Donald Trump amekutana na kufanya mazungumzo na Paul Kagame ambaye ni Rais wa Rwanda na  Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na kumuomba afikishe salamu zake za upendo kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi baada ya Mkutano wa Viongozi na Watu Mashuhuri Kuhusu Uchumi na Biashara Duniani, Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika.

Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana ambapo amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyakashifu mataifa ya Afrika huku akikiri kutumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.

Wakati wa mkutano wake na Kagame,  Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika huku akisifia kuwa mkutano wao huo ulikuwa “wa kufana sana”, na kueleza nchi hizo mbili kama washirika wa kibiashara ambao wanajivunia “uhusiano mzuri sana.”

“Ningependa kukupongeza, Bw Rais, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa … najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza karibuni. Tafadhali, fikisha salamu zangu.”

Rais Kagame alisema wameshauriana kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Marekani kwa Rwanda katika operesheni zake kote duniani, pamoja na masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na idadi ya watalii wa Marekani wanaozuru Rwanda, ambayo inaongezeka. Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa AU utafanyika kesho Jumapili na Jumatatu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot