MWANAHARAKATI wa kutetea haki za elimu nchini, David Msuya, ameshauri Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuangalia zaidi matatizo yanayokumba walimu na kutatua changamoto hizo na si kukimbilia kufungua kesi mahakamani.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, David alisema anatoa ushauri huo baada ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Halima Dendego, kutoa agizo la kuwavua vyeo walimu wakuu wa mkoa huo kutokana na kushuka kwa elimu mkoani hamu, lakini CWT imepinga ikitishia kwenda mahakamani endapo walimu hao watavuliwa vyeo.
Alisema hatua hizo zisichukuliwe kwa walimu pekee, bali hata kwa maofisa elimu wasiowajibika kwa kuvuliwe madaraka kwani wengi wao hukaa maofisini tu na hawaendi kuona na kuwasikiliza walimu kero zao maofisini.
"Hali hii inadhohofisha sana suala la elimu nchini, wakati mwingine maofisa wa elimu hawaendi kule mashuleni kusikiliza kero za walimu na hata wakifuatwa maofisini kwao, walimu hawapati nafasi ya kuwaona,"alisema David
Aliitaka Serikali kutowavumilia wafanyakazi wasiowajibika na si kwa walimu pekee bali hata katika taaluma zingine nchini
Aidha, alisema Sheria ya Maadili inasema mwajiri atatimiza wajibu wake kwa kumpatia mwajiriwa wake mshahara kwa kila mwezi na kwa wakati, lakini inaonekana kuwa kinyume kwani Sheria hiyo haitekelezwi
"Matatizo ya walimu ni mengi, changamoto ni nyingi siku hadi siku kama wao Chama cha walimu wanajua kutetea na kushughilikia kero ili ziishe na si kushabikia mambo,"alisema David
Alisema kuwa CWT inaonekana kuwa mtetezi wa walimu, lakini si kweli.
Aliongeza kuwa Mkuu wa Mkoa ni sawa na Rais kwenye eneo lake la utawala, hivyo akitoa tamko kama hilo linapaswa kusikilizwa na kutekeleza.
Alisema ni wajibu wa Tume ya Maadili kusikia agizo hilo na CWT ni wajibu wao kufanyia kazi kutokana na uzito wa jambo hilo.
"Mimi naunga kauli ya Mkuu wa Mkoa kuhusu kuvuliwa vyeo walimu wakuu na ikiwezekana mpaka kwa maofisa elimu wa Mkoa wa Mtwara ili kuendana na kasi ya Rais John Magufuli ya Hapa Kazi Tu,"alisema David
mwishooooooooooooooo



No comments:
Post a Comment