Mkazi wa kijiji cha Mwamgongo mkoani hapa Zubeda Said (33) anadaiwa kupigwa na mumewe hadi kuuawa baada ya kupoteza fedha yenye thamani ya shilingi 200.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini
hapa jana, dada wa marehemu, Siwema Masoud alidai kuwa awali ndugu yake
huyo alimpigia simu kuwa Januari 19 usiku alipigwa na mumewe kwa
kupotea Sh 200.
Alisema siku moja kabla alimpa mtoto wa
kaka yake mwenye umri wa miaka mitano Sh 200 akanunue maandazi, lakini
mtoto huyo aliporwa fedha hiyo na wenzake, akashindwa kurudi nyumbani
kwa siku mbili, akarudi siku ya ugomvi wa wawili hao na mumewe
kukasirika.
Alidai kuwa mume huyo, Kunduwenda Kiza
(37) akimfokea mtoto huvyo mama mtu kuamua kumwomba radhi mumewe huyo
lakini bila mafanikio kwani katika hali ya kushangaza mumewe alimpiga
mpaka kupoteza fahamu.
Siwema asilimulia kuwa kesho yake saa
9.45 alfajiri hali ya Zubeda ilibadilika na kutokwa damu sehemu
mbalimbali zilizo wazi mwilini mwake, mumewe akamkimbiza kwenye zahanati
ya kijiji hicho na Januari 20, alipewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa
ya Maweni.
Alisema Januari 21, saa 12.45 Zubeda
alipoteza maisha hali iliyowapa mashaka na kufikisha taarifa Polisi kwa
uchunguzi wa maiti lakini walipokwenda na askari hospitalini wakaambiwa
jalada halionekani.
Hata hivyo, mganga aliyetambuliwa kwa
jina la Dk Muganyizi alijitolea na kuufanyia uchunguzi mwili huo na
baada ya uchunguzi maiti alibaki mochari.
Lakini wakati ndugu wakijiandaa kwenda
kuchukua mwili walishangaa kukuta umeondolewa, na kwa msaada wa polisi
waliukamata ukisubiri kusafirishwa kinyemela.
Mwandishi alifika Maweni na kugundua
kuwa kabla ya kifo alilazwa wodi 2(b) ya wanawake huku jalada lenye
taarifa zake likiwa limetoweka huku uchunguzi wa Mganga ukibaini kuwa na
majeraha ndani ya mwili yaliyosababisha kuvuja damu kulikochangia kifo
hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ferdinand Mtui alikiri kupokea taarifa za kifo cha kutatanisha cha Zubeda.
Kamanda Mtui alisisitiza kuwa mshukiwa
Kiza anashikiliwa na Polisi kwa upepelezi na ikibainika ametenda kosa
hilo, atafikishwa mahakamani.



No comments:
Post a Comment