![]() |
| Mo pamoja na baadhi ya viongozi wa Simba pamoja na wageni waalikwa wakiwapungia mikono mashabiki waliojitokea kushuhudia mechi kati ya timu hiyo dhidi ya Sports Club Villa |
Mlezi na mnazi mkubwa wa Wekundu wa Msimbazi Simba Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘MO’ amenogesha tamasha la timu kwa hali ya juu ambapo kila wakati wa mashambulizi baadhi ya mashabiki walikuwa wakiimba na kutaja jina la MO.
MO
ambaye hadi sasa ameonyesha nia ya dhati ya kuitumikia klabu hiyo kama
mfadhili mkubwa wapo katika mazungunzo ya hatua mbalimbali kufikia hali
hiyo.
Timu
ya Simba katika mchezo ambao pia unaendelea sasa dhidi ya Sports Club
Villa, Wekundu hao wapo mbele kwa bao 2, zilizotupiwa kimiani na
mchezaji wake Ibrahim Hajibu ambaye alitupia bao la kwanza kipindi cha
kwanza na la pili katika kipindi cha pili tu cha mchezo huo.
![]() | |||
| Mlezi na mnazi mkubwa wa Wekundu wa Msimbazi Simba Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘MO’ akilishwa keki ya miaka 80 ya Wekundu hao wa Msimbazi |
![]() |
| Wageni waalikwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, MO, na Dk. Kigwangalla |
![]() |
| MO akisalimiana na mashabiki wa Simba baada ya mapunzimko. |








No comments:
Post a Comment