![]() |
| Rais wa Nchi ya Marekani, Barack Obama akiwa katika picha ya pamoja na Mgombea wa Urais wa chama hicho Bi. Hilalary Clinton. |
Na Carlos Nichombe
Rais wa Marekani Barack Obama
amemsifia mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton na kusema
ndiye anayefaa zaidi kuongoza Marekani na si Trump.
Akihutubu katika kongamano
kuu la chama cha Democratic mjini Philadelphia, huku akishangiliwa na
wajumbe, Rais Obama amesema hakujawahi kuwa na mtu aliyehitimu zaidi
kuongoza Marekani kuliko Bi Clinton."Hakujawahi kuwa na mwanamume au mwanamke, iwe mimi au Bill Clinton au mtu mwingine yeyote aliyekuwa amehitimu zaidi kuwa rais kama yeye kutokana na kuwa na sifa mbali mbali zinazomfanya awe tofauti na sisi tuliokwisha kuwa marais," amesema Bw. Obama.
Amemsifu pia kwa kujikakamua na kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya taifa hilo kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama kikubwa ambacho kimekuwa kikizingatia zaidi demokrasia nchini humo.
Amempongeza kwa kubomoa vizuizi mbali mbali vilivyowekwa na mifumo ya vyama na kuunda nafasi zaidi kwa Wamarekani hasa wanawake.
Amewaahidi Wamarekani kwamba Bi Clinton atatetea umoja na maadili ya Wamarekani ili yasiweze kushikiliwa na mtu mmoja pekee na kuifanya nchi hiyo kuwa na nguvu zaidi duniani katika nyanja ya kiuchumi na kisiasa.
![]() |
| Rais wa MarekaniBarack Obama |
Bw. Obama pia amemkosoa vikali mgombea wa chama cha Republican Donald Trump kwa kusema kuwa hatakiwi kuwa rais wa nchi hiyo na wananchi wa marekani wampigie kura mgombea wa cham chake kwani amekuwa na uzoefu kuliko wagombea wote walioingia katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.




No comments:
Post a Comment