| Ni Moja kati ya Basi ambalo timu ya Simba walipewa na wadhamini wao TBL |
Na Carlos Nichombe.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imeamua kutosaini mkataba wa kuendelea kuidhamini Simba.
Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinaeleza TBL imegoma kusaini mkataba ikionekana kuingia hofu baada ya Yanga kutotaka kuendelea nao au waingie wakiwa na ofa mpya.
![]() |
| Basi la Timu ya Yanga walilopewa na wadhamini wao waliomalizana nao mkataba, TBL |
Pamoja na hiyo imeelezwa kumekuwa na juhudi binafsi zinazofanywa na baadhi ya viongozi kujaribu kuwashawishi TBL kupitia Kilimanjaro, wabadili uamuzi.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele alisema jana mkataba huo na TBL unamalizika mwishoni mwa mwezi ujao na Simba haina mpango wa kuongeza tena.
Kahemele alisema kuwa makampuni kibao makubwa hapa nchini yanagombea kuingia mkataba na Simba na klabu hiyo inatafakari nani wa kuingia naye mkataba kutokana na fungu kubwa la fedha.
Alisema Simba ni timu kubwa na makampuni mengi yanataka kuingia nayo mkataba, hivyo ule wa TBL ulikuwa mdogo na unamalizika mwishoni mwa mwezi ujao.
Alisema baada ya kumalizika kwa mkataba huo, Simba itatangaza makampuni yanayotaka kufanya biashara na Simba.



No comments:
Post a Comment