Nay wa Mitego kifungoni - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, July 27, 2016

Nay wa Mitego kifungoni

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki 'Nay wa mitego'

Na Carlos Nichombe

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa muda usiojulikana msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Taarifa ya Basata kwa vyombo vya habari jana ilisema Nay atatumikia adhabu hiyo kuanzia jana hadi Basata itakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo yote aliyopewa.
Mbali na hilo, pia msanii huyo anaweza kutoka kifungoni pale baraza hilo litakapojiridhisha kwamba msanii huyo amebadilika na kubuni kazi zenye maadili na zisizodhalilisha watu wa kada mbalimbali.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki 'Nay wa mitego' akizungumza na Kituo cha matangazo cha mtandaoni cha millard ayo

Aidha, maagizo mengine aliyopewa msanii huyo ni kulipa faini ya Sh milioni moja, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasimishaji sekta ya Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na Basata na kuhakikisha wimbo wake umefuata taratibu zote.
Nay amekuwa akiingia matatani na baraza hilo mara kwa mara, mwishoni mwaka jana alisimamishwa kwa muda baada ya kutoa wimbo wa shika adabu yako ambao ndani yake aliwaimba baadhi ya wasanii wenzake wa muziki wa kizazi kipya na wa bongo movie.
Wimbo wake wa Pale Kati ndio uliokuwa gumzo tangu alipouachia takriban wiki mbili zilizopita ambapo video yake inaonekana kutokuwa na maadili kwa kuweka picha za wanawake zikionesha sehemu ya maungo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot