![]() |
| Mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette |
Na Carlos Nichombe
Klabu ya Lyon imekataa ombi la Euro milioni 35 kutoka kwa timu ya Arsenal kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wake raia wa Ufaransa Alexandre Lacazette.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 25 aliifunga mabao 21 timu hiyo katika mechi 34 msimu
uliopita na kandarasi yake inakamilika mwaka 2019.Katika taarifa yake katika mtandao wa Twitter,Klabu hiyo ya Ufaransa ilisema Lacazette hanunuliki na ni miongoni mwa viongozi wa timu hiyo ya kocha Bruno Genesio.
Lyon ilikana ripoti ya gazeti moja kwamba ilikataa ombi la Euro milioni 48 kutoka kwa klabu hiyo ya Uingereza na kusema kuwa hawakuwahi kupewa taarifa ya kuwepo kwa ofa ya aina hiyo iliyoripotiwa na gazeti hilo.



No comments:
Post a Comment