Apple kununua Tidal ya Jay Z - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, July 4, 2016

Apple kununua Tidal ya Jay Z


Jay Z akiwa na Mkewe.
Na Mwandishi Wetu
 
Kampuni ya Apple inadaiwa kutaka kuchukua umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki Jay Z 'Tidal'.

Kampuni hiyo imeripotiwa kwamba inaangazia wazo la kuinunua huduma hiyo kutokana na ushirikiano wake na wanamuzika bingwa kama vile Kanye West na Madonna.

Duru zimearifu jarida la Wall Street kwamba mazungumzo yameanza na huenda yakasababisha kupatikana kwa makubaliano.

Msemaji wa Tidal amekana kwamba imefanya mazungumzo na Apple na kuongeza kuwa wataujulisha umma pindi watakapokuwa wamefanya mazungumzo hayo.

Jay Z alizindua huduma hiyo mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kama mpinzani wa Spotify.


Jay Z akiwa pamoja na wadau katika kumiliki Kampuni hiyo.
Kampuni ya kiteknolojia ya Sweden, Aspiro ambayo ilikuwa ikiimiliki Tidal,ilinunuliwa na mwanamuziki huyo wa mtindo wa Rap kwa takriban dola milioni 56.

Jay Z aliandamana na Kanye West.

Alicia Keys na mkewe Beyonce ambao wote ni wadau katika kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot