TANROADS yaitaka Serikali kulipa fidia - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 13, 2016

TANROADS yaitaka Serikali kulipa fidia


Ni moja kati ya Barabara zunazoendelea kujengwa nchini



WAKALA wa Barabara Nchini(TANROADS) umeitaka serikali kuwalipa fidia wananchi walioko pembezoni mwa barabara zinazotakiwa kujengwa kwa wakati ili kuweza kukamirisha miradi ya ujenzi kwa wakati.

Akizungumza na waandishi wa habari  jana Jijini Dar es salaam Mhandisi wa miradi mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Ngusa Julius alisema miradi mingi inayoendelea hapa nchini imeshindwa kukamilika kwa wakati huku ulipaji wa madeni unaonekana kuwa ndio kikwazo kikubwa.

Alisema wamekuwa wakifanya jitihada kubwa kuweza kuwashinikiza serikali ili waweze kuwalipa wananchi waliopo pembezoni mwa barabara lakini ufinyu wa bajeti iliyokuwa ikitengwa kwa ajili ya masuala hayo ilikuwa ni ndogo.

"Tumekwishaanza miradi ya ujenzi wa barabara mbalimbali nchi nzima lakini kwa hivi sasa miradi mingi imesimamishwa kutokana na kuzuiliwa na wananchi wanaodai fidia za maeneo yao yanayopitishwa barabara na tunasubiri serikali ikamilishe mchakato wa malipo ili tuweze kuendelea na ujenzi wa barabara hizo" alisema Ngusa.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa TANROADS Aisha Malima amewataka wananchi kutunza miundombinu ya barabara zilizokwisha kamilika kujengwa ili kuweza kuzifanya barabara hizo kuwa endelevu na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachotengwa kwa ajili ya kufanya ukarabati wa barabara hizo.

Alisema kuwa uharibifu wa miundo mbinu mbalimbali iliyopo kwenye barabara imepelekea uharibifu wa barabara na kufanya tatizo la msongamano kuwa kubwa katika baadhi ya maeneo ya nchi hususani katika Jiji la Dar es salaam.

Hata hivyo Aisha aliwataka madereva na watembea kwa miguu kuzingatia alama zilizowekwa katika maeneo mbalimbali ya barabara ili kuweza kupunguza uharibifu wa miubdombinu ya barabara pamoja na kupunguza ajari zinazotokea hapa nchini.

Aliongeza kuwa katika kukabiliana na tatizo la foleni katika jiji la Dar es salaam wameanzisha miradi ya ujenzi na upanuzi wa barabara mbalimbali zilizopo baadhi ya maeneo ili kuweza kupunguza magari mengi kutumia barabara kuu na kupita katika barabara hizo za pembeni zinazoendelea kujengwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot