| Daktari wa Magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili akizungumzia hali ilivyo katika magonjwa hayo yanayolisumbua taifa. |
MAGONJWA yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo, kisukari na saratani yamezidi kuongezeka kwa kasi na kuendelea kuwa chanzo cha vifo duniani.
Hayo yalisema jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA) Dkt. Tatizo Waane,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu magonjwa hayo.
Alisema kuwa hivi karibuni kumekuwa naongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa,kama kisukari, kansa, shinikizo la damu,na uzito uliozidi.
Pia magonjwa haya yasiyoambukizwa chanzo chake kikubwa ni aina ya mifumo ya maisha tunayoishi yanachangia kwa kiasi kikubwa.
"Mifumo ya sasa ya maisha inafanya watu wengi kuingiza sumu nyingi sana kwenye miili yao,vyakula tunavyokula, kunywa au kuvuta vinaweza kuwa na sumu mbaya sana ambazo zitakusababishia magonjwa kama kansa,"alisema Dkt. Waane
Pia alisema kula vyakula vinavyotengenezwa haraka na vyenye kiwango kikubwa cha mafuta kunasababisha magonjwa kama presha na uzito uliozidi, Unywaji wa pombe na vinywaji vingine vinavyohifadhiwa kwa kemikali una sumu ambazo zinaathari kubwa kwenye mwili wako.
Pia Ili kuepukana na magonjwa haya lazima upunguza kabisa kutumia vyakula , vinywaji vinavyoweza kuwa na sumu,Kula mlo kamili Kwa mtu mzima unatakiwa kula mlo wenye mafuta kidogo, chumvi kidogo, wanga na protini kwa wastani na mbogamboga, matunda na maji kwa wingi sana.
"Kutofanya mazoezi nitatizo lingine kubwa linalochangia kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukizwa ni kutofanya mazoezi kwani Watu wengi hasa wanaokaa maeneo ya mjini na wanaofanya kazi za ofisini wanaongoza kwa kuwa na uzito uliozidi na kupata magonjwa kama presha na kisukari.
Hata hivyo alisema tunashauri mtu kupata angalau masaa mawili kwa wiki ya kufanya mazoezi na ukiweza kupata angalau nusu saa kila siku ya kufanya mazoezi inakuwa bora zaidi kwako.
Kwa upande wake Profesa Andrew Swai wa Hospitali ya Taifa Muhimbili alisema kuwa hapa Tanzania takribani watu tisa kati ya mia moja wana ugonjwa wa kisukari, huku mtu mzima mmoja kati ya watatu ana tatizo la shinikizo la juu la damu.
Alisema kuwa ugonjwa wa kisukari hutokama ma kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa na ikizidi husababisha madhara mengi kama kupata magonjwa ya moyo shinikizo la damu , kuharibu figo kwani kisukari ndiyo husababisha figo kushindwa kufanya kazi.
Pia alisema kuwa athari nyingine ya ugonjwa wa kisukari ni kupunguza nguvu za kiume na hivyo huharibu mahusiano ya ndani na karibu robo ya wanaume wote huwa na tatizo hilo wakishindwa kudhibiti kisukari.
Vile vile alisema ugonjwa wa kisukari huathiri uchumi kutokana na matibabu yake ni ya maisha na mahitaji ya dawa peke yake hayapungui sh. laki nne kwa mwaka kwa mgonjwa anayehitaji insulini.


No comments:
Post a Comment