![]() |
| Katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa, Mohammed Kiganja |
Hayo yalisemwa jana Dar Es Salaam na Katibu mkuu wa Baraza hilo, Mohammed Kiganja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumuaga Mchezaji bora wa Copa Coca-Cola msimu uliopita, Said Musa anayetarajiwa kuondoka leo kuelekea Ufaransa kwenye kambi ya Kimataifa iliyoandaliwa na Kampuni ya Coca-Cola.
Alisema kuwa kupelekwa kwa kijana huyo katika kambi hiyo itaweza kulisaidia taifa kukuza vipaji vyake kupitia mbinu mbali mbali ambazo kijana huyo atafundishwa na wakufunzi mbali mbali pindi awapo katika kambi nchini humo.
"Tunaamini kijana huyu atakuwa ni chachu ya maendeleo ya mpira hapa nchini kwa vijana wenzake kwani kupitia mbinu atakazozipata huko Ufaransa ataweza kuja kuwafundisha wenzake na hatimaye kuongeza idadi ya wachezaji wenye uwezo mkubwa hapa nchini kama vile walivyo akina Sammata" alisema Kiganja.
Aidha Kaimu Meneja Msaidizi wa Bidhaa na Masoko wa kampuni hiyo,Mariam Senziga alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kudhamini michuano mbali mbali hapa nchini ili kukuza tasnia ya michezo ambayo huchangia kukua kwa uchumi.
Alisema Jamii ijitokeze katika kuwahamasisha waweze kushiriki katika michezo kwani wanaamini kwa hivi sasa sekta hiyo imekuwa na heshima tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma ambako ilikuwa imedharauliwa zaidi.
Kwa upande wake Mshindi huyo wa Copa Coca-Cola Msimu uliopita, Said Musa alisema kuwa ataitumia kambi hiyo ili kuweza kuongeza kiwango chake na hatimaye awezekufikia ndoto alizojiwekea.
"Napenda niwaahidi Watanzania kwamba katika nafasi hii niliyoipata nitaenda kuitumia ipasavyo ili niweze kujifunza vitu vingi zaid ambavyo nilikuwa sivijui na kuongeza ujuzi zaid ya ule nilkiokuwa nao sasa" alisema Musa.
Musa anatarajiwa kusafiri hii leo kuelekea katika kambi itakayoanza kesho hadi Juni 4 itakayofanyika huko Jouy-En-Josas nchini ufaransa ambako anatarajiwa kurudi Juni 5.



No comments:
Post a Comment